MWENGE WA UHURU KUPOKELEWA GEITA KESHO

Mwenge wa Uhuru unatarajia kupokelewa Kesho, Tarehe 09 mkoani Geita ukitokea Mkoani Kagera ,ambapo utazindua na kupitia miradi 52 yenye thamani ya zaidi ya Sh Bil 18 ,ambapo miradi 8 itawekewa jiwe la msingi, mitatu itafunguliwa kumi na nne itazinduliwa na miradi 27 itakaguliwa na kuonwa.

Akizungumza mapema leo na waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema baada ya kukimbiza mwenge kwenye halmashauri tano zilizopo Mkoani Geita,mwenge huo utazimwa kitaifa Wilayani Chato.

“Tarehe 14 tunatarajia tukio la kuzimwa kwa mbio za mwenge litafanyika kwenye viwanja vya Magufuli na kuhuzuriwa na viongozi mbalimbali mgeni rasmi ambaye ndiye atahusika na shughuli ya kuzima ni Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan”---- Rosemary Senyamule Mkuu wa mkoa wa Geita.

No comments