FALLY IPUPA KUWASHA MOTO WA BURUDANI KESHO JIJINI DSM
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Fally Ipupa kesho anatarajiwa kutoa burudani ya aina yake katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ipupa amesema amejiandaa vya kutosha kuandika historia mpya ya muziki wa dansi.
Msanii huyo amesema mashabiki wake wajiandae kwenda kuburudika na kuwa kwa kipindi chote cha miaka 10 ambayo hajaja Tanzania ameandaa nyimbo nyingi ambazo zinapendwa.
Ipupa ambaye amewasili nchini hapo jana na kundi la wanamuziki zaidi ya 30 amesema mashabiki wake watakaonunua tiketi hawatajutia.
Alipouluzwa kuhusu athari za UVIKO 19 kwa kazi yake ya muziki Ipupa amesema iliathirika kutokana na mazingira ya ugonjwa huo kutaka watu wasisogeleane na katika maeneo mengine watu kulazimika kukaa ndani huku wengine wakipoteza maisha.
Akiwa nchini Ipupa atafanya maonyesho mawili ya muziki likiwemo la Oktoba 10 Dar es Salaam ambalo kiingilio chake ni Sh.100,000 kwa kiti na meza itakuwa Sh. milioni Moja wakati onyesho la pili likiwa ni Oktoba 13 jijini Mwanza kwa kiingilio cha sh. 50,000 kwa kiti.
Kwa Mlimani City milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 jioni.

Post a Comment