WAKAZI WA NSIMBO WALIA NA HALI TETE YA USALAMA
Wananchi wa Kata ya Kanoge Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameiomba Serikali kuingilia ili kukomesha matukio ya unyanyasaji vikiwemo vipigo, wanayofanyiwa na Viongozi wao wa Kata.
Hii ni kufuatia matukio ya mara kwa mara ya kupigwa kwa wananchi yanayowahusisha viongozi wa kata hiyo.
Katika tukio la hivi karibuni kabisa limetokea Oktoba 7, 2021 likimhusisha mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa majina ya Erneste Melkiore (45) aliyepigwa na watu wawili wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa majengo ya iliyokuwa shule ya msingi Nsanda.
Katika tukio hilo Melkiore anadai kuvamiwa na watu hao wakati akisafisha shamba lake lililopo jirani na majengo hayo na kisha kupigwa sehemu mbalimbali kabla ya kufungwa miguu na mikono kisha kufungwa nyuma ya pikipiki na kuburuzwa kwa umbali wa zaidi ya mita 200.
"Walinifunga kamba miguu na mikono, wakaniburuza umbali wa viwanja viwili vya mpira, baadae wakaanza kunipiga wakidai wanataka kunilainisha" alisema Melkiore
Aidha baada ya kichapo hicho Melkiore alitelekezwa kituo cha polisi Kanoge bila kuchukuliwa maelezo wala huduma yoyote mpaka alipochukuliwa ndugu zake na kukimbizwa katika kituo cha Afya Kanoge akiwa katika hali mbaya.
"Baada ya kunipiga walinipeleka kituo cha polisi, walidai wao ni walinzi wa msitu, askari aliwapigia simu watu wa maliasili (TFS) wakadai wao hawajawatuma na hawawatambui" alisema Melkiore
Katika tukio lingine linalofanana na hilo linamhusisha Joseph Bamila (60) lililotokea Agosti 15, 2021 baada ya mzee huyu kuchukuliwa nyumbani kwake usiku kupelekwa ofisi za kata na Afisa mtendaji wa Kata ya Nsimbo kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo wa Kata hiyo na kisha kupokea kipigo cha nguvu kilichomuachia kilema cha maisha.
Akielezea tukio hilo mzee Bamila amesema mpaka sasa haelewi sababu hasa ya yeye kufanyiwa unyama ule kwani hajawahi kushtakiwa kuhusiana na tukio hilo na hata waliomfanyia kitendo kile hawajashtakiwa licha ya yeye kulalamika.
Kufuatia matukio hayo wananchi wa kata hiyo wanadai kutokuwa na imani na serikali ya kata hiyo kwani katika matukio yote mawili na mengine yanayotokea viongozi wa serikali wamekuwa wakijitenga nayo.

Post a Comment