HARMONIZE ATINGA STUDIO YA MPENZI WA RIHANNA USA

Msanii wa muziki wa Tanzania, Harmonize au Konde Boy Mjeshi anaendelea kutisha na kuthibitisha msemo wake wa Konde Boy for everybody; akimaanisha Konde Boy ni kwa ajili ya kila mtu.

Harmonize ambaye ni C.E.O wa Konde Gang Music yupo nchini Marekani akiendelea na ziara 
za shoo zake tangu Agosti 15, 2021 ambapo ziara hizo atazihitimisha Januari, 2022. 

Mbali na kufanya shoo, akiwa nchini humo, Harmonize au Harmo amekuwa akiingia studio mbalimbali kubwakubwa kwa ajili ya kuandaa albam yake nyingine ambapo awali alifanya hivyo kule mjini Arizona, Marekani.

Studio hiyo ndiyo ambayo inatumiwa kwa sasa na mpenzi wa mwanamuziki wa kiwango cha dunia, Robyn Rihanna Fenty ambaye ni rapa mkubwa duniani aitwaye Asap Rocky.

Hata hivyo, Harmonize hakumkuta Asap Rocky, lakini alipata fursa ya kutumia vifaa ambavyo hutumiwa na staa huyo wakati akirekodi nyimbo zake.

Mastaa wengine wakubwa ambao waliwahi kutumia au hutumia studio hiyo pamoja na Rick Ross, Stef London ambaye ni mpenzi wa Burna Boy na wengine.

No comments