TFF KUFANYIA KAZI KASORO ZILIZOJITOKEZA MICHEZO YA AWALI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekutana na Klabu zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa ili kufanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika michezo ya awali.

Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) liliipiga faini dola za Kimarekani 5,000 Klabu ya Young Africans kutokana na klabu ya Rivers United kuripoti matukio ya kufanyiwa vurugu pamoja na kuonekana baadhi ya mashabiki katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ulitakiwa kuchezwa bila ya mashabiki.

Young Africans ilipata taarifa ya malalamiko ya Rivers United pamoja na uamuzi wa CAF kupitia TFF lakini haikujibu chochote.

Pia Tanzania ilipewa onyo kutokana na kuripotiwa kwa matukio mengi kwenye vyumba vya kubadili nguo pale vilabu vyetu vinapocheza mashindano ya Kimataifa na masuala ya vipimo vya PCR vya Uviko19 (Covid19).

Kupitia Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF Cliford Mario andimbo amesema Klabu zimetakiwa kuheshimu na kufuata kanuni, utaratibu na maelekezo ya CAF.

No comments