AMKA NA BWANA LEO 13/10/2021

*MSAFISHAJI WA KIUNGU.*

*Nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote. Isaya 1:25.*

▶️ Tunajaribiwa kwa kila njia mpaka taka na uchafu wote vitolewe kwetu, mpaka kisibaki chochote kilicho kichafu kwetu bali dhahabu safi. Kuna kazi inayopaswa kukamilishwa kwa ajili yako. Unapaswa kuwa na unyenyekevu wa kina wa roho na vita dhidi ya nafsi yako na nia isiyoyumbishwa, la sivyo utanaswa na adui.

▶️ Wale wanaopenda kusikia na kusema mambo wamekuhuzunisha, wamekujeruhi na katika akili yako umewashutumu wale ambao hawakustahili kukemewa na kutiliwa shaka na ulikuwa na mashaka na wale ambao ungeweza kuwaamini bila shaka. Unapotumia nafasi uliyopaswa, ndipo moyo wako utakapounganishwa sana na kaka na dada zako, na mioyo yao itaunganishwa na wa kwako, lakini umekuwa ukijitenga kutoka kwa ndugu zako na sababu iko ndani yako. Hauko tayari kuongozwa wala kuagizwa. Giza na mawingu vinakukusanyikia. Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano. Anaangalia kwa shauku kuu kuanguka kwako ili akufurahie.

▶️ Mungu analiita kanisa lake kutofautiana zaidi na ulimwengu katika mavazi yao zaidi ya ulivyodhania. Mungu anaendelea kuwaagiza watu wake wakimbie kutoka katika kiburi cha mwonekano, kutoka katika kujipenda nafsi, lakini moja kwa moja unafanya kinyume dhidi ya Roho wa Mungu katika jambo hili, kwa hiyo unatembea gizani na kujiweka kwenye uwanda wa vita wa adui.

▶️ Niliona kuwa Mungu anakupenda. Mchungaji mwema amekujali kwa upole na amekuhifadhi katikati ya maumivu na mateso ya akili, lakini lazima usalimishe nia na maamuzi yako na uwe tayari kufundishwa. Hakuna, hakuna hata mmoja, awezaye kwenda mwenyewe mbinguni. Mungu anao watu anaowaongoza, anaowaelekeza na anaowaagiza. Lazima wanyenyekeane wao kwa wao. Ikiwa mtu mmoja ataamua kwenda peke yake, bila wengine, atajikuta amechagua njia isiyo sahihi ambayo haitamwongoza katika uzima....

▶️ *Nimejitahidi kuliandika suala hili kama ambavyo liliwasilishwa kwangu. Ni ombi langu kuwa, uweze kuliona kama lilivyo na uhakikishe kuwa unafanya kazi kamilifu kwa ajili ya umilele.*

MUNGU ATUBARIKI SOTE.

No comments