SIRRO; WANAOPANGA MAANDAMANO TUTAWASHUGHULIKIA
"Nichukue fursa hii kuwapongeza nyinyi Wanahabari kwa kazi kubwa mnayoifanya kwa kuzingatia misingi ya Maadili ya Tasnia ya Habaria na Mawasiliano, Upendo, Uzalendo na Mshikamano wa Kitaifa kuwaelimisha na kuwahabarisha Watanzania"
"Aidha napenda kutoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha kutokana na changamoto za Janga la COVID -19, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina"
"Vile vile nawaombea kupona haraka na kurudi kwenye majukumu yao ya kazi wale wanaoendelea na matibabu kwenye hospitali mbalimbali nchini kutokana na changamoto hii"
"Hali ya Ulinzi na Usalama nchini ni shwari na inaridhisha ukiachilia mbali uhalifu wa hapa na pale ambao nao unakabiliwa vyema. Matukio makubwa ya Jinai na Usalama barabarani yameendelea kupungua kwa kiasi kikubwa"
"Ushwari huo umechangiwa na utekelezaji wa mara kwa mara wa Operesheni, Misako, Doria na
Ushirikishwaji wa Jamii kuanzia ngazi ya Familia, Wenyeviti wa Vitongoji. Mitaa na Vijyi, Watendaji Kata, Makatibu Tarafa, Wakurugenzi na Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya na Mikoa, Vikundi vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika kuhakikisha usalama"
"Hata hivyo, hivi karibuni kumezidi kujitokeza migogoro ya wakulima na wafugaji, migogoro hiyo imekuwa kero kubwa na wakati mwingine inahatarisha usalama kwa kusababisha mauaji na majeruhi"
"Vilevile kuna ongezeko la tabia ya watumiaji wa
Pikipiki maarufu Bodaboda kutovaa kofia ngumu (Helmet). Hali hii inasababisha vijana wengi na abiria wao kupata ajali hivyo kuongezeka lewa majeruhi na vifo"
"Kupitia nafasi hii naomba Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi zote zitusaidie kutoa elimu na kutatua migogoro kwenye himaya"
"Aidha ni vyema Halmashauri zote nchini zikahuisha sheria ndogo ndogo zitakazosaidia utatuzi wa migogoro na makosa ya waendesha bodaboda"
"Hivi karibuni Mwezi Mei-Juni, 2021 tulikuwa na operesheni kubwa kabisa nchini nzima baada ya kuwepo kwa viashiria vya uhalifu wa hapa na pale. Matokeo ya Operesheni ni kwamba tumefanikiwa kukamata watuhumiwa 5429 waliohusika uhalifu wa makosa makubwa ya Jinai kama vile, unyang'anyi wa kutumia silaha, unyang'anyi wa nguvu, wizi wa magari, mauaji, kubaka, kulawiti na dawa za kulevya za viwandani. Pia tumefanikiwa kukamata silaha 37, zikiwemo, Pistol 04, AK-47 01, Short Gun 03, Uzi Gun 01 na Magobore 29, Dawa za kulevya aina ya Heroine kg 540,
Cocaine Gram 458 Lita 13612.775 na Mitambo 94 ya kutengenezer Gongo na Waganga 15 wapig ramli chonganishi"
"Makosa ya Usalama Barabarani Kwa upande wa makosa makubwa ya usalama barabarani katika kipindi hicho cha operesheni ni 294, ajali za vifo ni 157, Watu waliokufa ni 211 na waliojeruhiwa ni
62, Kwa ujumla Makosa yamepungua kutokana na mwitikio chanya wa uti wa sheria bila shuruti kwa watumiaji wa vyombo vya moto kwa kuzingatia kanuni za usalama barabarani"
Operesheni Usalama VII,
"Kwa sasa tunaendelea na Operesheni Usalama VII kuanzia Julai 29,2021 Operesheni hiyo inahusisha nchi wanachama wa INTERPOL Ukanda wa Afrika
"Mashariki (EAPCO) na Kusini Mwa Afrika (SARPCO). Operesheni inalenga kukamata
watuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kupanga na unaovuka mipaka (Transinational Organised Crime) unaojumuisha:- Ugaidi, Wizi wa magari, Dawa za kulevya, Usafirishaji haramu wa binadamu, n.k. Mafanikio yaliyofikwa hadi sasa ni
kukamatwa kwa silaha Moja (01) AK 47, ikiwa na Magazine mbili (2) pamoja na Risasi 176 za AK. 47. Kufuatia operesheni hiyo pia imekamatwa Pistol moja (01)"
"Mnakumbuka mnamo tarehe 17-22/07/2021 mkoani Mwanza walikamatwa Wanachama/wafunsi 15 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Ndugu Freeman Aikael Mbowe, Wanachama hao walikamatwa kwa kosa la kutoa Matamshi yenye kuashiria
uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kuhamasisha/kushawishi wananchi kwa
vitisho na sharti kuwa lazima Katiba mpya ipatikane la sivyo, yanayoendelea Afrika Kusini (SA) yatatokea Tanzania"
"Baada ya kukamatwa Ndugu, Freeman Aikael Mbowe alipelekwa Jijini DSM ambapo
kulikuwa na kesi inayopelelezwa dhidi yake kuhusiana na kula njama na kufadhili
vitendo vya kigaidi. Watuhumiwa wenzake sita (6) walikuwa mahabusu na walishafikishwa mahakamani"
"Watuhumiwa wengine waliokamatwa Jijini Mwanza pamoja Ndugu. Mbowe waliachiwa kwa dhamana. Hata hivyo, baada ya upelelezi
kukamilika jalada la kesi litawasilishwa ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi"
"Kuhusu mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe na wenzake tuhuma dhidi yao kwa sasa iko chini ya Mamlaka ya Mahakama. Suala la dhamana kwa kesi wanayokabiliwa nayo nila kisheria na linasimamiwa na Mahakama"
"Hivyo, Jeshi la Polisi halitegemei mtu wala kikundi cha watu kwa namna yoyote kutoa shinikizo kwa mamlaka ya mahakama ama mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe aachiwe au
kupewa dhamana. Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi cha watu kitakacho jaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au kwa namna yoyote ile ili kutoa shindikizo lolote. Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama tumejipanga vizuri na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
ya watu hao."-----> IGP SIMON SIRRO, MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI
Post a Comment