MBUNGE MTEULE BW. SHEHA MPEMBA AJIUZULU
Mbunge Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Konde Mhe. Sheha Mpemba Faki Leo tarehe 02/08/2021 amejiuzulu nafasi hiyo.
Katika barua yake Mheshimiwa Sheha Mpemba Faki ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikafi na Uenezi Bw. Shaka Hamdu amesema Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM.
Post a Comment