WHO YAITAKA TANZANIA IPOKEE CHANJO YA CORONA
IKIWa ni siku moja tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kutaka Wizara ya Afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka Tanzania kujiandaa kupokea na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na Kanda ya Afrika mashariki kwa ujumla.
”Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla ” anasema Dkt. Moeti.
#BinagoUPDATES
Hatuitaki,waanze wao kwanza,sisi sio majaribio
ReplyDeleteUmenena,hakika
Delete