MAKATIBU TAWALA 30 WAAPISHWA LEO NA RAIS HUSSEIN MWINYI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo Agosti 2, amewaapisha Makatibu Wakuu mbali mbali aliowateua Julai 30 mwaka huu kushika nyadhifa hizo.
Katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu visiwani Zanzibar, Dk. Mwinyi amemuapisha Dk. Omar Dadi Shajak kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar pamoja na Bi. Khadija Khamis Rajab kuwa Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi na Uwezeshaji katika Wizara ya Nchi (OR) Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Aidha, amemuapisha Dk. Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Uchumi na Uwekezaji katika Wizara ya Nchi (OR) Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Mwingine aliyeapishwa ni Dk. Fatma Mrisho kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Dk. Hussein Mwinyi amemuapisha Ndugu, Khamis Kona Khamis kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar,kufuatia uteuzi wake wa tarehe 16 Julai 2021.
#BinagoUPDATES
Post a Comment