IDADI YA WAKURUGENZI WANAWAKE YAFIKIA 55
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. @ummymwalimu amesema Uchambuzi wa awali wa Uteuzi wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan unaonyesha kuwa Wakurugenzi 70 wamehamishwa vituo vyao vya kazi na Wakurugenzi 45 wameendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi.
"----->Wakurugenzi 69 ni wapya kati ya hao Wakurugenzi 15 wamejaza nafasi zulizokuwa wazi na Wakurugenzi 54 wamechukua nafasi za Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa"---- UMMY MWALIMU
Aidha Waziri Ummy pia amebainisha kuwa Uchambuzi wa awali unaonyesha kati ya Wakurugenzi wapya 69 wanawake ni 33 sawa na asilimia 48 hivyo kufanya idadi ya Wakurugenzi wanawake kuwa 55 sawa na asilimia 29 ya Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Post a Comment