BASHUNGWA AWATAKA BAKITA KUACHANA NA NJIA ZA KIZAMANI
“BAKITA amkeni achaneni na njia za kizamani, tumieni njia za kielekroniki sasa hivi ulimwengu umehama upo mtandaoni, Idara ya TEHAMA kazeni buti, mtu wa nchi za nje atapataje machapisho yenu kama hamuwekei mkazo katika kutoa taarifa kupitia mitandao?” Amesema Bashungwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa maagizo hayo leo Agosti 2, 2021 Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika ofisi za Baraza la Kiswahili Nchini (BAKITA) na kuwaagiza kuanza kutumia njia mpya yakujitangaza na kutangaza lugha ya Kiswahili nchini na kuachana na mifumo ya kizamani na kujikita kuanzisha vituo vya mafunzo ya Kiswahili katika Balozi zetu mbalimbali duniani ili kuunganisha lugha ya Kiswahili na sekta ya Utalii kukuza hiyo pamoja na Utamaduni wa Tanzania.
Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa alitembelea darasa la kisasa la kufundishia Wakalimani ambalo limefungwa vifaa vya vioya vya kisasa ambalo bado halijafunguliwa rasmi kwa sasa.
Kwa upande wao BAKITA wamemuelezea Mhe. Waziri mipango yao ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 ikiwemo kuongeza idadi ya wakalimani 50 nchini ili kukidhi hitaji la wakalimani ili kukidhi tija ya huduma hiyo nchini.
Post a Comment