MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA PENTEKOSTE NZEGA
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kusimamia uhuru wa kuabudu kwa kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuheshimu uhuru huo wa ibada zinazoendeshwa katika nyumba za dini na itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini na madhehebu yote kwa ajili ya ustawi wa taifa na watu wake.
Amesema hayo leo (Jumapili 29 Agosti 2021) Alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu wa Muungano wa Makanisa ya Umoja wa Pentekoste Tanzania Elieza Isaka Mazinge, katika kanisa la Pentekoste Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.
“----->Pale mtakapo pata tatizo lolote linalohitaji kutatuliwa na Serikali waoneni viongozi wa Serikali walioko katika maeneo yenu, Maelekezo ya serikali ni lazima viongozi hao waunge mkono jitihada za dini katika kufanya taifa hili kuwa tulivu.”---- MAJALIWA
Post a Comment