MAJALIWA AAGIZA MAGOGO YALIYOKAMATWA YAUZWE-TABORA
Agizo hilo limetolewa jana Agosti 28, 2021 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa anazungumza na wakazi wa Kijiji cha Wachawaseme wilayani Kaliua.
Waziri Mkuu ameshangazwa na shehena kubwa ya Magogo yaliyokatwa maeneo hayo na kusema hakuna Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake anayeweza kuharibu mazingira kwa kukata Magogo.
"Kama kweli we ni Mtanzania na una uchungu, kuithamini na kuipenda Nchi yako kamwe huwezi kufanya hivi nina shaka," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Amewataka wananchi kutunza mazingira na kuachana na Tabia ya kuyaharibu huku alishangazwa na Kasi ya uharibifu mkubwa wa mazingira,Akisema hilo haliwezekani na watu watunze mazingira.
Amewaambia wakazi hao kuwa wana dhamana ya kuyalinda na kuyatunza mazingira na kuachana na tabia ya kupuuzia utunzaji mazingira.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amemweleza Waziri Mkuu kuwa Magogo hayo yalikatwa kwa njia isiyo ya kawaida.
Akitoa historia ya Magogo hayo, amesema yalivunwa kwenye maeneo ya mapori yanayozunguka vijiji kumi na moja vinavyounda hifadhi ya Isawima bila kufuata utaratibu na wahusika kutojulikana.
Amesema magogo hayo yalibainika kuvunwa pasipo kufuata taratibu na Serikali ya mkoa ikatoa kibali yatolewe maporini na kukusanywa kwa gharama za Serikali ya Wilaya na vijiji.
Amesema kwa vile yalikatwa kwenye maeneo ya wazi ambayo Serikali kuu inayasimamia, ilitoa amri ya kuyataifisha ambapo sasa yakiuzwa, gharama ilizotumia Serikali za vijiji na wilaya, zitarudishwa na ziada kuingizwa Serikali kuu.
Naibu Waziri huyo amewataka wakazi hao kuwa mstari wa mbele kulinda Maliasili inayowazunguka kwa manufaa yao na Taifa.
Waziri Mkuu hadi jioni hii, alikuwa eneo la hifadhi ambapo magari yanayotumiwa na watalii ndio yaliingia na wengine kubaki kusubiri
Post a Comment