MAKUBI: KUFIKIA 28/08/2021 WATU 304,604 WAMEPATIWA CHANJO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi amesema Serikali inaendelea kuratibu utoaji wa
chanjo ya UVIKO-19 (COVID-19) kupitia vituo vya kutokea huduma za Afya vya umma na binafsi
vilivyoidhinishwa hapa nchini.
Tathmini ya zoezi la utoaji wa chanjo Prof. Makuhi amesema inaonesha mpaka kufikia tarehe 28.08.2021, jumla ya walengwa 304,603 wamepatiwa chanjo, kati ya hawa walengwa,
201,476(66.1%) ni wanaume na 103127(33.9%) ni wanawake.
"----->Ili kuongeza kiwango na kasi ya wananchi kupatiwa huduma hii ya chanjo pasipo usumbufu,
naendelea kuelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, kuhakiksha kuwa idadi ya vituo
vinavyotoa chanjo vinaongezwa na kuanzisha huduma mkoba, ili kutoa urahisi zaidi wa wananchi kupata chanjo pasipo usumbufu wa kusafiri umbali mrefu, vilevile katika vituo vyote, watoa huduma wote, waendelee kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kila mteja watakaye mhudumia kwa magonjwa mengine ili kumpa nafasi ya uelewa na baadae yeye kuchukua maamuzi sahihi juu ya chanjo"---- MAKUBI
Amewataka Wananchi waliofika kuchanjwa, wapewe elimu zaidi ya chanjo pamoja na kufahamu hali zao za kiafya na maudhi ya kawaida ambayo yanaweza kutokea kwa baadhi yao wachache.
"Ikumbukwe pia kwamba zoezi la utoaji wa chanjo linaenda sambamba na kutoa cheti kwa kila
mteja anayechanjwa"
"Vyeti vyetu vipo katika aina mbili, cheti cha mfumo na cha kawaida kwa maeneo ambayo hayana mtandao"
"Tayari Wizara ilishatoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa Mikoa na halmashauri kuwasilisha taarifa za wananchi ambao walipata chanjo kabla ya kuanza kutumia mfumo ili wataalamu wetu wa TEHAMA ngazi ya wizara waweze kutoa vyeti vya mfumo kwa wananchi hao na kuwaondolea usumbufu wanaoupata punde wanapohitaji kutumia vyeti hivyo, Hivyo naelekeza tena kwa mara nyingine kuwa taarifa hizi tuzipate si zaidi ya tarehe 01.09.2021 siku ya Jumatano"
"Mwisho, Wizara pamoja na kupongeza mamlaka za Mikoa, Wilaya na Mitaa kwa kuhamasisha
zoezi la chanjo, pawepo pia na juhudi zaidi za kuongeza kasi katika maeneo ya pembezoni ya miji na vijijni"
"Aidha nawaasa Wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote za kinga dhidi ya UVIKO-19 kwa kunawa mikono na maji tiririka/kutumia vipukusi, kuvaa barakoa katika maeneo hatarishi,
kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima na kufanya mazoezi kila mara"
Post a Comment