EWURA YASITISHA UPANDAJI WA BEI ZA GESI MAJUMBANI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imebaini uwepo wa baadhi ya kampuni za gesi ya kupikia majumbani (LPG)
kupandisha bei za gesi hiyo kiholela.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo, Mhe. Godfrey H. Chibulunje amesema EWURA ina jukumu la kulinda maslahi ya wateja kwa mujibu wa Kifungu 30(2)O(1) na 30(2)(d) cha Sheria ya Petroli, Sura. Na 392; na Kifungu 6(b) cha Sheria ya EWURA, Sura Na. 414.

Hivyo basi, EWURA imeagiza kusitisha mara moja upandishwaji wowote wa bei ya gesi ya kupikia majumbani mpaka pale itakapopokea na kupitia mapendekezo na hoja za uhalali wa kupandishwa kwa bei hizo.

Pamoja na agizo la kusitisha kwa bei hizo, kampuni za uuzaji wa gesi ya LPG zinapaswa kuwasilisha EWURA maelezo ya uhalali wa ongezeko la bei hiyo mara moja, kwa ajili ya uhakiki ili EWURA iweze kuthibitisha pasipo shaka juu ya uhalali wa upandaji wa bei hizo. 

Kampuni yoyote itakayoshindwa kutekeleza maagizo haya ya kiudhibiti itachukuliwa hatua za kisheria, kwa mujibu wa Chibulunje.


No comments