AMKA NA BWANA LEO 5
*KESHA LA ASUBUHI.*
Alhamisi, 05/08/2021.
*KUFUNIKWA NA HAKI YA KRISTO.*
*Tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; Wafilipi 3:9.*
▶️Yoshua, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana na mavazi machafu, anawakilisha wale ambao maisha yao ya kidini yamekuwa na makosa, ambao wameshindwa na majaribu ya Shetani, na hawastahili fadhila ya Mungu. Leo wansimama mbele za Mungu wakiwa na mavazi machafu. Haki yao yote ni "kama nguo iliyotiwa unajisi" (Isaya 64:6). Shetani hutumia dhidi yao nguvu zake stadi za kushtaki, akielekeza kasoro zao kama ushahidi wa udhaifu wao. Anasonda kwa dharau makosa ya wale wanaodai kumtumikia Mungu. Wamedanganywa naye, na anaomba ruhusa ya kuwaangamiza.
▶️Lakini wanamtumainia Kristo, na Kristo hatawatelekeza. Alikuja katika ulimwengu huu ili kuondoa dhambi zao, na kuwahesabia haki yake. Anatangaza kwamba kupitia imani katika jina Lake wanaweza kupokea msamaha, na kukamilisha tabia kama ya Kristo. Wamekiri dhambi zao kwake, na wameomba msamaha, na Kristo anatangaza kwa sababu wanamtegemea na kumwamini, atawapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu.
▶️Tabia zao zina kasoro, lakini kwa sababu hawajatumainia kustahili kwao wao wenyewe na kutoa udhuru kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu wameomba msamaha kupitia stahili za Kristo, Bwana anawapokea, na kumkemea Shetani. Kwa sababu wamejinyeyekeza, wakikiri dhambi zao, Yeye anakataa kusikiliza mashtaka ya adui. Amewasamehe kabisa wale waliotubu, na ndani yao ataendeleza mbele kazi Yake ya upendo wenye kukomboa ikiwa wataendelea kumwamini na kumtumainia.
▶️ *Wale ambao, kwa neema ya kiungu, wamepata ushindi juu ya makosa yao, wanapaswa kuwafundisha wengine jinsi ya kushinda, wakiwaelekeza kwa Chanzo cha nguvu. Kwa kila nafsi iliyoongoka kunatolewa fursa ya kuwasaidia wale walio karibu naye ambao hawaifurahii nuru ile ambayo kwayo anasimama. Wao pia wanaweza kujua furaha ambayo imemjia. "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;" (Yohana 1:12). Wanaweza kuchukua nafasi zao ulimwenguni kama wabeba nuru wa Mungu.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment