MCHEPUKO

Uchumba usio na mwisho
Ni rahisi sana kwa wanaume kuanza kuwapuuzia wake zao mara tu baada ya ndoa. Kabla ya ndoa , mwanaume hufanya juhudi sana na hutumia nguvu nyingi kujaribu kumfurahisha na kumpata mkewe-mtarajiwa. Huingia katika uchumba kwa shauku kubwa na kudhamiria sana kama mwanariadha wa Olympic. Humpatia mwenzi wake umakini wote na kumfanya kuwa kitovu cha shuauku yake. Pale ndoa inapokamilika , mwanariadha wetu anageukia malengo mengine. Anatambua kuwa , sehemu ya mapenzi katika maisha yake sasa iko chini ya utawala wake , na sasa anaondoka kwenda kukwea milima mingine ya maisha. Sasa anatumia muda mchache na mchache kuwa na mkewe , na kumtendea kana kwamba si mtu muhimu saaanaaa. Wakati huohuo , mrembo wake aliyezoea  mchakato wa uchumba , anaingia katika ndoa AKITEGEMEA MAMBO YALE YALE aliyozoeshwa kipindi cha uchumba. Kadri, ndoa inavyoendelea , mrembo anajikuta akijikita Zaidi na Zaidi kumuelekea mumewe kuliko ilivyokuwa kabla ya ndoa , wakati ambapo mumewe akijikita kidogo na kidogo tena kumuelekea mkewe. Sasa mrembo anamfulia nguo , anampikia chakula , anamtandikia kitanda , anamsafishia nyumba , na huenda anampangia nguo kwenye begi. Wakati huohuo mumewe, anapunguza kujali( japo anaongeza mihemko) , yaani anapunguza kumtoa out , kiujumla haonekani kujali saaana.

Hili gonjwa , likiendelea pasipo kutibiwa , mara nyingi linazua mchepuko. Michepuko kama ilivyozoelewa kusomwa katika riwaya(novel) ,  na ile inayoigizwa na Hollywood na kwenye TV , sasa imekuwa gonjwa la taifa. Wakati mmoja katika huduma yangu , nilikuwa nashauri wenzi 16 ambao walikuwa na changamoto za kindoa zinazohusisha michepuko. Katika kila kesi , niliuliza swali hili “Nini kilikuvutia kwa huyu mtu/mchepuko? Katikakila kesi majibu yalionekana kufanana , walijibu “ Huyu mwanaume alinifanya nijisikie kama mwanamke?’’ AU “ Huyu mwnamke alinifanya nijisikie kama mwanaume tena/again?” Ni rahisi kumfanya mwanamke ajisikie hivi wakati wa uchumba. Sio rahisi kufanya hivi wakati wa ndoa. Haiwezekani kumfanya mkeo ajisikie kuthaminiwa kiasi hiki kama mke anatazamwa kama jambo lisilo muhimu saaaana. Wakati Paulo anaongea kuhusu umuhimu wa waume kujitoa kwa wake zao kama Kristo alivyojitoa kwa kanisa , Paulo anaguza kabisa moyo wa ndoa. [R.C.Sproul, The Intimate Marriage , pp.42-43}. MOJA YA FUNGUO MUHIMU YA KULINDA NA KUDUMISHA NDOA YAKO NI KUTOMPUUZIA MKEO NA KUDUMU KUMCHUMBIA.
               PMC 360 : 2021

For more
Download Application yetu ya Binago Tv 👉📱 play store sasa..We are social.. follow us on social media📺

1 comment: