AMKA NA BWANA LEO 3

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumanne, 03/08/2021.

*NGUVU YA UKWELI.*

*Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Isaya 58:6.*

▶️Ukweli, ukweli wa thamani kubwa, unatakasa katika mvuto wake. Utakaso wa roho kwa utendaji wa Roho Mtakatifu ni kupandikiza asili ya Kristo katika ubinadamu. Ni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kudhihirishwa katika tabia, na neema za Kristo kuletwa katika utendaji hai katika kazi zilizo njema. Hivyo tabia hubadilishwa kuwa kamilifu zaidi na zaidi kufanana na sura ya Kristo, katika haki na utakatifu wa kweli. Kuna masharti  mapana katika ukweli wa kiungu yanayojitandaza na kuungama katika mstari mmoja baada ya mwingine wa kazi zilizo njema. Kweli za injili hazijatengana; kwa kuungana zinaunda safu moja ya vito vya thamani vya mbinguni, kama ilivyo katika kazi binafsi ya Kristo, na kama nyuzi za dhahabu zinapita katika kazi na uzoefu wote wa Kikristo.... 

▶️Hebu chapa na ipigwe akilini kwamba rehema na upendo wa Mungu vinapaswa kuoneshwa kwa watoto wa Mungu. Chunguza mbingu na dunia, na hakuna ukweli uliodhihirishwa kwa nguvu zaidi ya ule unaooneshwa katika huruma kwa wale hasa ambao wanahitaji huruma yako na msaada kwa ajili ya kuvunja nira, na kuwaweka huru walioonewa. Hapa watu wauishi ukweli huo, ukweli huo unatiiwa, ukweli huo unafundishwa kama ulivyo katika Yesu.

▶️Kuna ukweli mwingi ambao watu wanaukiri, lakini unaotumika kuwafariji wanadamu wenzetu una mvuto mkubwa, unaofika hadi mbinguni, na kuenea katika umilele. Kila roho katika ulimwengu wetu inajaribiwa; uzoefu wa kila mtu, historia ya kawaida ya maisha, inaeleza kwa lugha dhahiri kama ni yeye mtendaji wa maneno ya Kristo na kazi Zake. Daima kunajirudia safu za mambo madogo madogo ambayo ni Mungu peke yake huiona; kutenda kanuni za ukweli katika mambo haya kutaleta thawabu yenye thamani kubwa. Mambo makubwa na muhimu hutambuliwa karibia na watu wote, lakini kuunganishwa pamoja kwa mambo haya na mambo yale ya maisha yaliyo madogo madogo na kuviunganisha kwa karibu kuwa kama kitu kimoja, hufanywa kwa nadra sana na wale wanaodai kuwa Wakristo. 

▶️ *Ukweli wa kiungu huwa na mvuto mdogo kwa wanadamu wenzetu, wakati ambapo ulipaswa kuwa na mvuto mkubwa kupitia katika utendaji wetu. Ukweli, ukweli wa thamani kubwa, ni Yesu maishani, kanuni hai, inayotenda kazi.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

Download app yetu 👉📱play store sasa

No comments