WAZIRI ABIY AHMED ASHINDA UCHAGUZI ETHIOPIA

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda katika mashindano yake ya kwanza ya uchaguzi, lakini hana sababu ya kusherehekea, kutokana na hali mbaya ya nchi hiyo, kulingana na wachambuzi wa nchi hiyo wanavyosema.

Jumamosi, bodi ya uchaguzi ilitangaza ushindi wa kishindo wa chama cha Waziri Mkuu Abiy Ahmed katika shindano lake la kwanza la uchaguzi.

Baada ya miezi kadhaa nyuma, pamoja na kucheleweshwa mara mbili,  Ethiopia imekuwa na uchaguzi wake.

Hapo awali ilipangwa mnamo Agosti 2020, iliahirishwa hadi Juni 5 kwa sababu ya janga la coronavirus. 

Ilicheleweshwa tena ili kuwezesha muda zaidi wa kushughulikia shida za uandikishaji wa wapiga kura na changamoto zingine za uchaguzi katika nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, mwishowe ilifanyika mnamo Juni 21.

No comments