WAUGUZI WATAKIWA KUWAHUDUMIA WAGONJWA KWA UPENDO
Wahitimu wa ngazi mbalimbali za uuguzi wametakiwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaokuja kupata matibabu katika vituo vyao vya kazi.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kibaha Dkt. Gunin Kamba aliyemuwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe katika mahafali ya pili ya wauguzi waliohitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya wauguzi kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Dkt. Gunin Amesema taaluma ya uuguzi ni muhimu sana katika kuboresha afya za wananchi hivyo kila muhitimu ametakiwa kuwa na wito wa kutoa huduma kwa upendo na weledi.
"Nipende kutoa wito kwenu nyie wahitimu na wauguzi wote kwa ujumla kuwa uuguzi ni kazi ya wito, upendo na weledi wa hali ya juu. Hivyo zingatieni maadili ya taaluma kwani mgonjwa anapolazwa anamtegemea muuguzi kwa uangalizi wa karibu". Amesema Dkt. Gunin.
Nae msajili wa baraza la wauguzi Bi. Agnes Mtawa amesisitiza wauguzi wote wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini kujisajili katika baraza hilo na kupewa cheti na hati ya utambulisho.
Bi. Agnes amesema kumekua na baadhi ya wauguzi wasiokua na vyeti na usajili wa baraza hilo lakini wamekua wakitoa huduma mtaani. Hivyo kupitia mfumo wa usajili waliweza kubaini wauguzi 50 ambao walikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria huku wengine wakihukumiwa kwenda jela.
Wauguzi kutoka vyuo mbalimbali nchini wapatao 2713 wa ngazi mbalimbali walitunukiwa vyeti vya kuhitimu pamoja na usajili.

Post a Comment