AMKA NA BWANA LEO 26
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumatatu, 26/07/2021.
*KWA KADIRI YA IMANI YAKO.*
*Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Mathayo 9:29.*
▶️Ni wajibu wetu, kama watoto wa Mungu, kuzungumza imani, na wala si shaka. Tunapaswa kuwa na matumaini na wenye furaha katika Bwana. Hebu na tusiangalie upande wa giza wa hali, bali tuangalie juu, na kumwamini Yule ambaye Mungu alimtoa kwa ulimwengu ili apate kutuokoa kutoka katika dhambi zetu. Kristo anatimiza wokovu wetu kwa kuweka mvuto wa kuwa na imani mioyoni mwetu na kuusadiki ukweli. Ukweli unaweka huru; na wale ambao Mwana huwaweka huru wako huru kweli kweli. Hebu na tujitahidi kumheshimu Mungu kwa kudhihirisha daima imani inayozidi kuongezeka katika uhakikisho kwamba ataikubali kila roho inayomtumikia kwa uaminifu.
▶️Sisi ni watoto wadogo wa Bwana, na tunapaswa kuongozwa na kushikiliwa Naye. Ikiwa tutajifunza masomo kutokana na huruma na uvumilivu na upole wa Yesu, tutakuwa baraka kwa wote ambao tutashirikiana nao. Bwana angetamani kwamba tufarijiwe na ahadi zake, na kumsifu zaidi kuliko tunavyofanya. "Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza" (Zaburi 50:23). Hebu na tujifunze jinsi ya kuonesha shukrani zetu kwa Mungu kwa sababu ya kujishusha kwake kwa jinsi ya ajabu na upendo kwa wanadamu.
▶️Mwana pekee wa Mungu alikubali kuondoka katika nyua za mbinguni na kuja katika ulimwengu wetu huu apate kuishi na watu wasio na shukrani ambao walikana rehema Zake. Alikubali kuishi maisha ya umaskini, na kuvumilia mateso na majaribu. Akawa Mtu wa huzuni na anayejua sikitiko. Na Neno linatangaza, "Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao" (Isaya 53:3). Kati ya wanafunzi Wake mwenyewe, Petro, alimkana, na Yuda alimsaliti. Watu ambao alikuja kuwabariki walimkataa. Walimtia katika fedheha na kumsababishia mateso yasiyoelezeka. Waliweka juu ya kichwa chake taji ya miiba iliyotoboa uso wake mtakatifu. Walimpiga kwa mjeledi, kisha wakamsulubisha msalabani. Lakini bado katikati ya yote hayo, hakuna neno lolote la kulalamika lililotoka midomoni mwake....
▶️Kristo alichukua mateso haya yote ili apate haki ya kuwatumikia haki ya milele watu wengi kadiri ya wale ambao wangemwamini. Ninapolifikiria hili, ninajisikia kwamba hakuna lalamiko hata moja linapaswa kutoka katika midomo yangu....
▶️ *Pale tunapopatwa na shida, hebu na tutafakari jinsi wokovu wetu ulivyomgharimu Mungu wa ulimwengu.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOZIDI KUWA NA IMANI THABITI KATIKA YEYE.
Post a Comment