MUONGOZO WA UDHIBITI WA UGONJWA WA CORONA (UVIKO-19)
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi ametoa mwongozo wa kudhibiti ugonjwa wa Corona bila kuathiri shughuli za kiuchumi.
Prof. Makubi amesema kuwa mwongozo huo unaelekeza kusitishwa kwa mikusanyiko mikubwa isiyo ya lazima jambo litalosaidia kuvunja mnyororo wa maambukizi katika Jamii.
Ameendelea kusema kuwa, mwongozo huo unaelekeza endapo italazimika shughuli hizo kutendeka basi ni lazima kiombwe kibali kutoka Halmashauri na hatua zote za kujikinga zifuatwe ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa.
Hata hivyo, ameelekeza elimu itumike ili wananchi waweze kubadilika pasipo matumizi ya nguvu.
Kisha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya Wataalamu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji safi tiririka, kuvaa Barakoa na kuepuka msongamano isiyo yalazima.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi, Wamiliki wa vyombo vya usafiri, madereva na Mamlaka husika kuhakikisha kuepuka kusongamana (abilia wasisimame) kwenye mabasi, na kuhakikisha wanavaa Barakoa wakati wote wawapo ndani ya basi.
Kwaupande wa mwendokasi amesema kuwa, abilia waepuke msongamano kwa kuhakikisha wanakaa mita moja kati ya abilia mmoja na mwingine, huku akisisitiza ni lazima kunawa mikono kabla ya kupanda basi na kuvaa Barakoa muda wote.

Post a Comment