PROF. MAKUBI; TUMESHATOA NJIA ZA KUJIKINGA NA CORONA
Tayari Serikali kwa ujumla wake, kuanzia Mhe. Rais, Mhe. Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wetu wa Afya na viongozi wengine mbalimbali, tumeshatoa matamko mbali mbali kuhusiana na kuelimisha wananchi na kuwaelekeza jinsi gani wanaweza kujikinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, ikiwemo jinsi ya kukabiliana na misongamano na kuiepuka hasa hasa misongamano isiyo yalazima"
Ni kauli ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akiongea na Waandishi wa habari katika mwongozo wa kudhibiti ugonjwa wa Corona bila kuathiri shughuli za kiuchumi, katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam
Aliendelea kusisitiza kuwa ni vema wananchi wote wakawa wasikivu na kutii maelekezo ya viongozi na watalaamu kwa kufuata afua zote za kinga ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji safi tiririka, kutumia vitakasa mikono (sanitizers), kuvaa barakoa, kuepuka misongamano isiyoyalazima, kufanya mazoezi, kuzingatia lishe, kuendelea na matumizi ya dawa asilia, kuwakinga wazee na wagongwa, na matumizi ya Chanjo.

Post a Comment