USIYOYAJUA KUHUSU NGUVU YA MAOMBI
1. Maombi ni kinga dhidi ya Shetani.
Biblia Inasema:-
"Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.." (waefeso 6:11-12)
2. Maombi humwokoa Mwenye dhambi:
Biblia Inasema:-
"Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi" (Luka 10:13)
3.Maombi huponya wagonjwa.
Biblia Inasema:-
"Na kule Kuomba kwa Imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua, hata ikiwa amafanya dhambi, atasamehewa"
(Yakobo 5:15)
4:Maombi hukamilisha Yale yasiyowezekana.
Biblia Inasema:-
" Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata.”
(Mathayo 21:12)
5. Maombi hugawanya au hutoa hekima.
Biblia Inasema:-
" Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa" ( Yakobo 1:5)
6.Maombi hutupatia vitu vizuri.
Biblia Inasema:-
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye huona, naye abishaye atafunguliwa."
(Mathayo 7:7-8)
7.Maombi hubadilisha wakati au nyakati.
Biblia Inasema:-
" Nenda ukamwambie Hezekia, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa baba yako Daudi, anasema hivi: Nimesikia ombi lako na nimeyaona machozi yako. Basi, nakuongezea miaka kumi na mitano ya kuishi."
( Isaya 38:5)
8.Maombi husaidia Wengine ikiwa tutaomba kwa ajili yao.
Biblia Inasema:-
"Ninyi nayi mkisaidiana nasi kwa ajilinyetu Katika Kuomba, ili, kwa Sababu ya Ile karama tupewayo sisi kwa Msaada wa watu wengi, watu wengi watoe Shukrani kwa ajili yetu"
( 2 wakorintho 1:11)
9.Maombi huonyesha Nguvu ya MUNGU
Biblia Inasema:-
"Kisha Elia akajinyosha juu ya mtoto huyo mara tatu na kumwomba Mwenyezi-MUNGU, “Ee Mwenyezi-MUNGU, Mungu wangu, mrudishie mtoto huyu roho yake!” Mwenyezi-MUNGU akasikiliza ombi la Elia; mtoto akaanza kupumua tena"
( 1 wafalme 17:21-22)
10.Maombi hutoa Amani.
Biblia Inasema:-
"Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu."
( Wafilipi: 4:6-7)
BWANA AKUBARIKI 🙏🙏
Imeandaliwa Na:-
Psychologist & Counselor
Mwl, sunzu 💭
Post a Comment