AMKA NA BWANA LEO 24
*PANDA KANDO KANDO YA MAJI.*
*Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake. Mathayo 10:7-10.*
▶️Paulo, mtume mkuu wa Mataifa, alijifunza ufundi wa kutengeneza mahema. Kulikuwapo na madaraja ya juu na ya chini ya utengenezaji wa mahema. Paulo alikuwa amejifunza madaraja ya juu, na pia aliweza kufanya kazi katika madaraja ya kawaida, wakati ilipolazimu....
▶️Wayunani kwenye pwani ya bahari walikuwa wafanya biashara hodari. Walikuwa wameelimika katika desturi ya kufanya mapatano katika biashara, na waliamini kuwa faida ni utauwa, na kwamba uwezo wa kupata faida, iwe kwa njia nzuri au mbaya, ulikuwa ni sababu ya kufanya waheshimiwe. Paulo alikuwa anafahamu desturi yao, na hakutaka kuwapa nafasi ya kusema kwamba yeye na awatendakazi wenzake walihubiri ili kupata riziki kutokana na injili.
▶️Ingawa ilikuwa sawa kabisa kwake yeye kupata riziki kwa njia hii(kwa kuwa "Mtenda kazi wa astahili ujira wake"), lakini aliona kwamba ikiwa angelazimika [kufanya hivyo], mvuto kwa watendakazi wenzake na wale ambao aliwahubiria usingekuwa bora. Paulo aliogopa kwamba kama angeishi kutokana na kuhubiri injili, angeweza kushukiwa kuwa na nia ya ubinafsi kwa wale ambao walihubiri neno. Hakutaka kuwapa Wagiriki hodari nafasi yoyote ya kuharibu mvuto wa watumishi wa Mungu.
▶️ *Paulo aliwaza, Angeliwezaje kufundisha amri, ambazo zilimtaka ampende Mungu kwa moyo, na kwa roho, na kwa nguvu, na kwa akili, na jirani yake kama yeye mwenyewe, kama angempa mtu yeyote sababu ya kufikiri kwamba alikuwa anajipenda yeye mwenyewe kuliko jirani yake au Mungu wake, kwamba alifuata desturi za Wayunani, akifanya biashara kwa uhodari katika kazi yake kwa ajili ya kupata faida, badala ya kufuata kanuni za injili. Angewezaje kuwaongoza watu kwa Kristo, ikiwa angechukua vyote ambavyo angeweza kupata kutoka kwao? Paulo aliamua kwamba asingewapa wafanyabiashara hawa wenye bidii, walio wakosoaji, wasio wanyofu fursa ya kudhani kwamba watumishi wa Mungu walikuwa wakifanya kazi kwa uhodari ili kujinufaisha kama wao na kufuata njia zisizo za uaminifu kama zao.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.
Post a Comment