UMMY MWALIMU APIGA MARUFUKU MICHANGO KIDATO CHA 5

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,  Mhe. Ummy Mwalimu  amepiga  marufuku kwa Mkuu yeyote wa Shule kutoza michango Kwa mwanafunzi anayejiunga na kidato cha Tano katika shule za Serikali,2021 zaidi ya Shilingi 188,000 ikijumuisha na Ada Shilingi 70,000.

Amesisitiza kuwa atakayekiuka Agizo hili atachukuliwa hatua.

"Kila la heri kwa Kidato cha 5 mwaka 2021/22. Michango na Ada ya mwaka kwa Shule zote za Serikali isizidi Tshs 188,000/=." ----> UMMY MWALIMU

No comments