"Sasa hoja yetu ikawa sawa wale watu waliandamana je maandamano yalisababishaje kifo cha Akwilina? Walifanyaje?
Sasa hivi hukumu imewaachia huru akina Mbowe wito wangu kwa wale wote wenye Mamlaka ambao wanalifuatilia suala hili wafanye juhudi waweze kuwaambia wananchi ukweli nini hasa kilitokea kuhusu yule binti (Marehemu Akwilina). Ni kidonda ni lazima kitibiwe kama tume iundwe kwa sababu kwenye mahakama jibu halijatolewa kwamba kwamba Akwilina alifariki vipi, sasa kwa kuwa Mahakama imewaachia huru akina Mbowe lile swali kuhusu Akwilina alifariki vipi inatakiwa lijibiwe" Wakili Peter Kibatala.
Wakili Kibatala ameyasema hayo, akiwa MBASHARA Clouds TV.
0 Comments