WAFANYABIASHARA WADOGO KUZINGATIA SHERIA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka amefanya mkutano mkubwa na Wafanyabiashara Ndogo ndogo Mkoani Dodoma kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na ametumia fursa hiyo kuelekeza viongozi wa Serikali wa kuanzia mamlaka za chini kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara hao na badala yake wawe sehemu ya kuwawezesha kukua kibiashara na kufikia malengo yao.

Aidha Mh Mtaka pia amewataka wafanyabiashara hao wadogo wadogo kuzingatia sheria na kanuni za kufanya kwao biashara ili wasilete athari kwa wananchi wengine wakati watimiza majukumu yao.

Katika mkutano huo wafanyabiashara wadogo waliiomba serikali iwapange vizuri katika maeneo hayo na kurasimisha baadhi ya maeneo ili wasipate bugdha kutoka kwa Askari na migambo wa Jiji.

Mkutano huo uliowakutanisha Wafanyabiashara wadogo kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma,pia yalihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dr. Fatma Mganga,Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma,Wakuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde

No comments