UHAMISHWAJI WATEJA KUTOKA (D1)KWENDA KUNDI (T1)
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuomba radhi kwa usumbufu uliyojitokeza kwa baadhi ya wateja baada ya hatua ya kuhamishwa toka kundi la wateja wenye matumizi madogo ya umeme yasiyozidi unit 75 kwa mwezi (01) kwenda kundi la wateja wenye matumizi ya kati yanayoanzia unit 75 kuendelea kwa mwezi (T1).
Tayari Uongozi wa Shirika umeagiza ofisi zote za TANESCO mikoa na wilaya kuwarudisha wateja
wote waliohamishwa kimakosa na kuzingatia mwongozo wa bei elekezi ya umeme ya TANESCO
"TANESCO Tariff Adjustment Order" (Kupitia GN. Na. 119) ya mwaka 2016 na marekebisho yake
kupitia GN Na. 1020 ya mwaka 2020, inayosimamiwa na EWURA.
Aidha, ofisi za TANESCO zinahakiki upya wateja wote waliohamishiwa kundi la T1 ili kujiridhisha
kama walifikia kigezo cha kuhamishiwa kwenye kundi hilo kwa mujibu wa Sheria na taratibu.
Uhamisho wowote wa wateja kutoka T1 kwenda D1 hufanyika pale mteja atakapoleta maombi
katika ofisi ya TANESCO kwa barua, wakati uhamisho wa kwenda T1 hufanywa na Shirika pindi mteja anapozidisha matumizi ya unit 75 kwa miezi mitatu mfululizo, hata kama mteja hajaleta
maombi ya kuhamishwa.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliyojitokeza kwa wateja na watumiaji wote wa
huduma za umeme nchini.
Post a Comment