TFF YAJIRIDHISHA, YATOA ADHABU YANGA, SIMBA
Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichokutana Julai 27, 2021 kilipitia taarifa za mchezo Fainali ya kombe la Shirikisho (ASFC) uliochezwa Julai 25, 2021 katika Uwanja wa lake
Tanganyika, Kigoma.
Kamati imejiridhisha kwa mujibu wa kanuni na kutoa adhabu kwa makosa mbalimbali.
KWA UPANDE WA SIMBA SC
(i)Klabu ya Simba imetozwa faini ya shilingi 2,000,000 kwa kosa la viongozi Viongozi na Washabiki kukaidi maelekezo, walilazimisha kuingia Uwanjani na kupita kwa nguvu mlango
usio Rasmi wakati wa zoezi maalum la kutembelea uwanja wa mazoezi na kusababisha Uharibifu wa mali, vurugu kinyume na kanuni ya 45:1, adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa
Kanuni ya 45:25.
(ii) Timu ya Simba SC imetozwa faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 15:54 kwa kosa la Viongozi kuingia uwanjani kwa kutumia mlango Usio Rasmi, Viongozi wa Simba walitumia mlango wa vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji kuingia uwanjani (pitch area) wakiambatana na watu mbalimbali miongoni mwao wasiokuwa na tiketi za kuingia Uwanjani kinyume na utaratibu.
(ii) Klabu ya Simba SC imetozwa faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 45:1 kwa mashabiki wake kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kusababisha vurugu na askari wa uwanjani wakati wa mapumziko kwenye
eneo la Vyumba vya kuvalia (Changing Rooms) kinyume na utaratibu.
(iv) Klabu ya Simba Pamoja na Viongozi husika wamepewa Onyo kali kwa mujibu wa Kanuni ya 38:5 kwa kukaidi maelekezo, kuvuruga na kuingilia kinyume na utaratibu uliokuwepo kwenye shughuli za Utoaji Medali/Zawadi kwa Wash-
indi wakijua kuwa hawakuwa sehemu ya Utaratibu huo kinyume na Kanuni ya 44.9.
(v) Mchezaji wa Simba SC Bernard Morrison alifanya kosa la kimaadlili, kinidhamu na udhalilishaji kinyume na kanuni ya 39:20, amefungiwa kucheza michezo mitatu ya timu yake na faini ya shilingi ya 3,000,000.
KWA UPANDE WA YOUNG AFRICANS
(i) Klabu ya Young Africans ilivunja Kanuni ya 15:15 kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani imetozwa faini ya shilingi 1,000,000 kwa mujibu wa kanuni ya 15:54 ya
Kanuni za Ligi Kuu.
(iI) Young Africans ilivunja kanuni ya 45:1 ambapo Watendaji/washabiki wake walijihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa mwamuzi wa akiba wa mchezo wakati wa mapumziko kinyume na utaratibu, imetozwa faini ya shilingi 500,000.
(iii) Viongozi wa Young Africans waliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, walitumia mlango wa mashabiki jukwaa la Urusi kuingia uwanjani (pitch area) wakiambatana
na watu mbalimbali miongoni mwao wasiokuwa na tiketi za kuingia Uwanjani kinyume na utaratibu, imetozwa faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 15:54.
(iv) Mashabiki wa Young Africans waliwashambulia waamuzi wa mchezo huo kwa chupa za maji kwa nyakati tofauti wakati wa mchezo kinyume na utaratibu, Young Africans imetozwa faini ya shilingi laki 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 15:54.
(v) Viongozi na Washabiki wa timu Young Africans walikaidi maelekezo, walilazimisha kuingia Uwanjani na kupita kwa nguvu mlango usio rasmi wakati wa zoezi maalum la kutem-
belea uwanja wa mazoezi na kusababisha Uharibifu wa mali, Vurugu kinyume na Kanuni ya 45:1, imetozwa faini ya shilingi 2,000,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 45:25.
(vi) Mukoko Tomombe alitenda kosa kumpiga John Bocco kinyume na kanuni na taratibu, amefungiwa kutocheza michezo mitatu ya timu yake na faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 39.5.
(vii) Farouk Shikalo kwa makusudi alikwepa kusalimiana na waamuzi na wachezaji wa timu ya Simba kinyume na Kanuni ya 15:13 ametozwa faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 15:54.
(viii) Kocha wa Young Africans Mohamed Nasreddine Nabil aligoma kuhudhuria Mkutano wa maandalizi ya Mchezo na Waandishi wa Habari kinyume na kanuni na Utaratibu, ametozwa faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya
43:2.13.
NINI MAONI YAKO MDAU..?✍
Post a Comment