BABU WA LOLIONDO AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kijiji cha Samunge Mkoani Arusha zinasema Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kama "Babu wa Loliondo amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa kutoka kwa Ndugu na majirani wanasema aliugua kwa muda wa siku nne mpaka alipofikwa na mauti siku ya Leo akiwa nyumbani kwake

Babu wa Loliondo alipata umaarifu mkubwa kutokana na Dawa yake iliyofahamika kama Kikombe cha babu kudaiwa kutibu maradhi sugu mbalimbali jambo ambalo lilivutia wananchi wengi miaka kumi iliyopita.

Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile alikuwa akiishi katika kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro ikiwa ni kilomita 450 kutoka Arusha mjini.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema peponi, Amin

No comments