SIMBA SC, GOR MAHIA ZAKATWA KUSHIRIKI KAGAME CUP

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC na miamba ya soka nchini Kenya, GOR Mahia
wamekatwa kati ya miongoni mwa timu kumi
zilizothibitishwa kushiriki Kombe la Kagame la
CECAFA kwa mwaka huu 2021.

Mnyama ndio Bingwa wa kihistoria wa Michuano hii ya vilabu ukanda wa CECAFA akinyakua mara sita.

Mashindano haya yatachezwa jijini Dar Es Salaam
yataanza tarehe 1 na kufikia tamati 15 mwezi Agosti 2021.

KCCA ya Uganda ndio mabingwa watetezi wa michuano na watashiriki kwasababu hiyo huku
Express FC itashiriki katika mashindano ya mwaka huu kama Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda.

Kutoka Tanzania Bara, kutakuwa na timu mbili
ambazo ni mabingwa mara tano wa mashindano,
Yanga SC na Azam FC ambao ni mabingwa mara
mbili na kutoka visiwani Zanzibar kutakuwa
muwakilishi mmoja ambaye ni klabu ya KMKM.

Miamba ya Soka kutoka nchini Malawi Nyassa
Big Billets ndio timu mualikwa..

Wakati timu nyingine kutoka CECAFA zipo Tusker FC ya Kenya hawa wana mataji matano ya michuano hii, APR FC ya Rwanda, Atlabara FC Sudan Kusini na Le Messager Ngozi kutoka Burundi - Droo ya mashindano hayo itafanyika Jumanne, 27 Julai 2021 na kutakuwa na makundi mawili na vilabu vitano katika kila kundi.

No comments