PROF. MAKUBI; UPIMAJI JOTO UENDELEE KUTEKELEZWA KWA UFANISI
Upimaji wa joto ili kutambua dalili ya COVID-19 katika maeneo mbalimbali ya shughuli za kijamii uendelee kutekelezwa kwa ufanisi ili kutambua hali ya Afya ya wananchi wanaofika katika maeneo hayo kupata huduma za kijamii, hususan upimaji katika maeneo ya usafiri wa mabasi, katika maeneo ya masoko
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu mwongozo wa kudhibiti ugonjwa wa Corona bila kuathiri shughuli za kiuchumi. Shughuli imefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam.
Aidha, ameelekeza maeneo yote ya kuabudu kama vile makanisa na misikiti kuwekwa vyombo vya kunawia mikono na vitakasa mikono (sanitizer), huku akiwataka waumini kufuata kanuni zote za kujikinga dhidi ya Corona ikiwemo kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu, kuvaa Barakoa na kunawa mikono kwa sabuni na maji safi tiririka au kutumia vitakasa mikono.
Ameendelea kwa kushauri kuwa, ibada zifanyike kwa muda mfupi na kama haitaathiri kitu basi zifanyike katika maeneo ya wazi ili kupata hewa ya kutosha kwa waumini wao jambo litalosaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Post a Comment