FREEMAN MBOWE AZIDIWA, POLISI WAKATAA KUMPELEKA HOSPITALI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema leo Jumatatu tarehe 26 Julai, 2021 kimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambao walimtembelea Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay asubuhi hii.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mwenyekiti Mbowe anaumwa na tayari ameshalijulisha Jeshi la Polisi kuhusu kuumwa akiwataka wampeleke hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi na matibabu.
CHADEMA, wamesema mpaka Muda huu Polisi hawajampeleka Hospitali Kwa ajili ya vipimo na matibabu.
Aidha CHADEMA, imewaelekeza Mawakili wake kufika mara moja kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kumuona Mwenyekiti.
"----->Tunalitaka Jeshi la Polisi limpeleke Hospitali mara moja kwani ni haki ya mtuhumiwa kupatiwa matibabu kwa mujibu wa Sheria za Tanzania."---- CHADEMA
Post a Comment