ALIYEMTEKA MO DEWJI AACHIWA HURU LEO
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia Kesi na kumwachia huru Dereva Taxi, Mousa Twaleb aliyekuwa akishitakiwa kwa kumteka Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji maarufu kama 'MO'
Twaleb alifikishwa Mahakamani hapo May 28, 2019 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, ambapo ilidaiwa katika shitaka la kwanza Mshitakiwa alijihusisha na genge la uhalifu.
MO alitekwa Oktoba 11, mwaka 2018 alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo majira ya usiku alipotelekezwa na gari katika eneo la Gymkhana.

Post a Comment