MAWETE MUSOLO BADO NI MALI YA SIMBA QUEENS

Meneja wa klabu ya Simba Queens, Seleman Makanya amesema nyota wa timu hiyo Flaviane Mawete Musolo bado yuko nchini kwao DR Congo na hajajiunga na timu kutokana na matatizo ya kifamilia huko Kinshasa.

Makanya alisema mchezaji huyo ataungana na wenzake kwenye michuano ya CECAFA WOMEN CHAMPIONS LEAGUE QALIFIERS yatakayofanyika Nairobi nchini Kenya Julai 17 hadi Agost 1 mwaka huu.

No comments