MAOMBI YENYE UWEZO

*MAOMBI YENYE UWEZO WA KUFIKA MBELE ZA MUNGU KIRAHISI*

Sehemu ya nne.

*4.MAOMBI YA KUTAFUTA*

Biblia inasema hivi

*👉Mathayo 7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye ATAFUTAYE huona; naye abishaye atafunguliwa.*

👆🏻Kwenye haya maandiko utaona Yesu anasema hivi *👉Naye atafutaye huona*

✔Kwahiyo *“kuomba upewe”* ni kitu kingine na *“kutafuta ulichokiomba”* ni kitu kingine pia

✔Wengi wanajua kuomba ni kweli lakini hawajui kutafuta walichokiomba ikiwa wameomba kwa mda mrefu bila kupata majibu, ndiyo maana kwasababu hawatafuti walichokiomba hujikuta wanatembea bila majibu ya maombi yao..

*➡Ukitaka uone sharti ni moja tu UTAFUTE*

*➡Wewe utapandaje mazao halafu usirudi kutafuta ulichokipanda kama kinaota au la?*

✔Ni hivi, Kibiblia kile tunachokiomba kinapaswa kuwa chetu.

*👉MARKO 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.*

✔Pia kibiblia lolote lile tunalomwomba Mungu tunapaswa kulipokea.

*👉1 YOHANA 3:22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.*

👆🏻Kwahiyo kama ahadi ya Mungu ni kuwa tunayomwomba tunayapokea au yanakuwa yetu, basi tambua yakwamba si mpango wa Mungu wewe ukiomba usijibiwe.

*➡Hivyo basi, ukiona unaomba kwa mda mrefu haupati majibu inaweza ikawa ni kwasababu hautafuti ulichokiomba, yaani hatufuti NENO LA MUNGU KWA HABARI YA KILE ULICHOKIOMBA ndiyo maana HAUONI MAJIBU YA MUNGU*

🔶Maombi ya kutafuta ni maombi ya kipekee sana.

*🔶NDANI YA MAOMBI YA KUTAFUTA NDIPO UNAPOPATA YAFUATAYO*

1.Ukiingia kwenye maombi ya kutafuta unapata ufunuo wa neno la Mungu wenye kukupa majibu ya kile ulichoomba..

✔Ndicho kilichotokea kwa habakuki, 👉Habakuki alipoona hapati majibu ya maombi yake aliamua kutafuta neno la Bwana juu ya kile alichokuwa akiomba kwa mda mrefu na baada ya kutafuta, Bwana akampa majibu kupitia NDOTO.

*◾HABAKUKI 2:1-3 BHN*

*👉1 Mimi nitasimama mahali pa kuchungulia, na kukaa juu mnarani; nitakaa macho nione ataniambia nini, atajibu nini kuhusu lalamiko langu.”*

*2 Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi: “Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma.*

*👉3 Maono haya yanangoja wakati wa kufaa; ni maono ya ukweli juu ya mwisho. Kama yaonekana kuchelewa, uyasubiri; hakika yatafika, wala hayatachelewa.*

👆🏻Haya ndiyo matokea ya kutafuta

*➡Kwahiyo, ukitafuta Mungu anakupa kuona neno lake lenye majibu ya kile ulichomwomba*

2.Ukiingia kwenye maombi ya kutafuta, unajua sababu ya kwanini Mungu amechelewa kujibu maombi yako au kwanini hakupi kabisa unachomwomba.

*➡Wayahudi walipopigwa vitani Yoshua alienda kuomba maombi ya kutafuta majibu ya kwanini wakapigwa vitani na alipoomba Mungu akamjibu yakuwa ni kwasababu ya dhambi iliyo juu yao ndiyo maana wakapigwa*

Fuatana nami katika maandiko yafuatayo👇.

*◾YOSHUA 7:6-7& 10-12*

*6 Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.*

*7 Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng'ambo ya Yordani*

*10 Bwana akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?*

*11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.*

*👉12 Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.*

👆🏻Haya ndiyo matokeo ya kuomba maombi ya kutafuta..

*👉Kama Yoshua asingetafuta sababu ya wao kushindwa vitani jiulize ingekuwaje❓*

✔Huenda wana wa Israeli wangemwona Mungu wao ni mwongo na ahadi zake kwao ni za uongo ndiyo maana hajawasaidia vitani,

✔Lakini Pia wangeendelea kuangamia kwasababu hawajui chanzo

*➡Hivi ndivyo walivyo wapendwa wengi, hujikuta wanamlalamikia Mungu kana kwamba hawaoni, wanamwona Mungu kama amewaacha, mbaguzi au hayupo kwasababu tu hajawajibu maombi yao👈 malalamiko yote ya aina hii ni matokeo ya kutofanya maombi ya kutafuta*

✔Kwahiyo usilizike tu kuomba kwa mda mrefu ukaishia hapo, jifunze pia kutafuta neno la Mungu juu ya kile ulichoomba kwa mda mrefu bila majibu ili utembee na majibu ya Mungu kwa habari ya maombi yako.

*➡Narudia tena kuomba upewe ni kitu kingine na kutafuta ulichoomba kwa mda mrefu bila majibu ni kitu kingine hivyo jifunze kutafuta pia ulichoomba*

🔶KUMBUKA.

*✔Tunatafuta majibu ya maombi yetu baada ya kuomba kwa mda mrefu bila kupata majibu au NENO LA MUNGU JUU YA HICHO TULICHOKIOMBA*

🔶JINSI YA KUFANYA MAOMBI YA KUTAFUTA

*✔Ni kumwomba Mungu aseme neno tu juu ya mahitaji yako ili wewe UPONE.*

Imeandikwa hivi👇

*👉LUKA 7:7 kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.*

👆🏻Baada ya maombi haya Mungu anaweza kukupa neno kupitia ndoto, maono, mahubiri, maandiko n.k..

MWISHO..

*👉YEREMIA 29:13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.*

JE UNATAKA UONE MAJIBU YA MUNGU JUU YA MAOMBI YAKO?  WEWE TAFUTA UTAONA.

Kwa leo niishie hapa hadi kipindi kijacho

Mungu wa mbinguni awabariki sana🙏

WhatsApp +255657117595

Mwl.Joseph Leonard

No comments