AMKA NA BWANA LEO 28
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumatano, 28/07/2021.
*THAWABU KWA UAMINIFU.*
*Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo. Luka 21:34.*
▶️Mpendwa rafiki Mkristo, tulia na ufikiri. Unafanya biashara na pesa za Bwana wako; nawe unazitumia kwa matumizi gani? Unaweza kutesa akili yako kushughukishwa na mapatano ya kibiashara na masumbufu ya maisha haya; lakini hutaweza kuvibeba vitu hivi kwenda navyo katika ule ulimwengu mwingine. Hakutakuwa na matumizi ya aina hii ya elimu kule. Basi kwanini usitumie talanta zako kuujenga ufalme wa Kristo? Kwanini usitoe katika kazi ya Mungu busara, ustadi, na nguvu ambayo imekufanya kuwa na mafanikio katika biashara? Kazi za ulimwengu huu zitaharibiwa. Je! Haingekuwa bora kuweka sehemu ya nguvu zako za kufikiri katika kusudi la Mungu, na kujenga mahali pale ambapo kazi itakuwa ni ya kudumu, nawe hutapata hasara?
▶️Mzigo wa daima wa mioyo yenu unapaswa kuwa, Nifanye nini ili kuokoa roho ambazo kwa ajili yake Kristo alikufa? Kote kunizunguka kuna roho za thamani kubwa zinazokaa katika uovu, ambazo lazima zitapotea kama mtu hatafanya kazi kwa ajili ya wokovu wao. Ninawezaje kuwafikia kwa jinsi ilivyo bora hawa wanaotangatanga, ili nipate kuwaleta kwenye mji wa mtukufu wa Mungu, na kuwawasilisha mbele ya kiti cha enzi, nikisema, Mimi hapa na watoto ambao Bwana amenipa?
▶️Wengine wanaweza kujitetea kwa kusema, sikuwa na uzoefu katika aina hii ya kazi; Nimetumia uwezo wangu katika vitu vya maisha haya tu. Sawa, ni juu yako kusema kama utaendelea kutumia muda wako na nguvu kwa ajili ya masilahi ya kidunia, au utavitumia katika kusudi la Mungu. Hakuna hata mmoja atakayelazimishwa kuingia katika huduma hii. Ikiwa tutachagua kuleta pamoja nguvu zetu juu ya mambo ya kidunia, hakutakuwapo kitu cha kutuzuia. Lakini kwanini tunaendelea kuweka hazina hapa badala ya juu? Chukulia kwamba utapaswa kubadili utaratibu wa mambo, na kuweka sehemu ya hazina yako mbinguni, je usingelifurahi kuipokea tena badaye, na bila kuharibika?
▶️ *Kristo amempangia kila mtu kazi yake. Mauti ya pili itakuwa ni fungu la wale ambao hawafanyi kazi, na maneno ya kuogopesha yatasikika, "Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mathayo 7:23). Lakini watumishi waaminifu hawatapoteza thawabu yao. Watapata uzima wa milele, na maneno "Vema, mtumishi mwema na mwaminifu" (Sura ya 25:23), yatasikika kama muziki mtamu masikioni mwao.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment