MAKAO YA WATAKATIFU
Miaka ya nyuma Marekani ilitumia
mabilioni ya dola kutuma watu mwezini. Hata sasa wapo wanaotumaini kuchunguza sayari nyingine ambako hakuna matatizo kama tuliyo nayo hapa duniani. Lakini kutafuta dunia nyingine hakutatatua matatizo ya mwanadamu. Mbegu za ubinafsi, uovu, ukatili zimo ndani ya moyo wa kila mmoja wetu. Je, tunawezaje kupata amani na usalama katika
dunia hii? Je, kuna matumaini ya hali bora zaidi katika siku za usoni? Je, hakuna mahali ambapo hatutazeeka, mahali ambapo tutaishi kwa amani
na furaha kamili? Kuna nchi ya namna hiyo. Kuna kitu bora
zaidi m bele yetu. Mungu amewaandalia wale wampendao mahali bora zaidi. Hili ndilo tumaini
ambalo limewatia nguvu watu wa Mungu katika karne zote.
Hebu tuone Biblia inavyosema kuhusu mambo mazuri ambayo Mungu amewaandalia watu wake
wa ufalme wmbao atausimamisha.
1. Mungu amewaandalia nini watu wake?
“Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao, maana amewatengenezea mji.” Ebr. 11:16. Mungu amewaandalia watu wake mji.
2. Mji huu ambao Mungu ameuandaa uko wapi?
“Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.” Ufu. 21:2. “Ee BWANA, Mungu wangu… sikia huko mbinguni, makao yako.” 1 Fal. 8:28-30.
3. Je, mji huo wa ajabu ukoje?
A. Ukubwa
“Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi;
ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.”
Ufu. 21:16. Mzunguko wake ni maili 1500. Hii ni sawa na kilomita 2400. Upande mmoja ni kilomita 600.
B. Jina
“Yerusalemu Mpya” Ufu. 21:2.
C. Kuta Zake
“Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne… Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi.” Ufu. 21:17,18.
D. Milango
“Ulikuwa na… milango kumi na miwili,… Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa
kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu… Na ile milango kumi na miwili ni lulu
kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja.” Ufu. 21:12,13,21.
Milango 12 – kila upande matatu – kila moja limetengenezwa kwa lulu moja.
E. Misingi
“Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili,… imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho;
wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.” Ufu. 21:14-20.
Mji una misingi kamili 12 – kila mmoja umejengwa kwa kito cha thamani – kila rangi iliyo kwenye upinde wa mvua itakuwapo. Hivyo kwa mbali mji utaonekana kama vile uko juu ya upinde wa mvuo.
F. Barabara
“Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.” Ufu. 21:21.
Barabara zitakuwa za dhahabu safi,
zikiakisi utukufu wa mbinguni kama kioo.
G. Mwonekano
“Mji ule mtakatifu,… umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”
“Wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama
kito cha yaspi, safi kama bilauri.” “Marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.”
Ufu. 21:2,11. Mji utakuwa unang’aa kwa utukufu wa Mungu. Uzuri wake unafananishwa na bibi-arusi
aliyepambwa kwa ajili ya mume wake.
4. Ni jambo gani la ajabu ambalo litawahakikishia wakazi wa mji
huu nguvu na ujana milele zote?
“Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,
wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.” Ufu. 22:2. “Akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele.”
Mwa. 3:22. Mti wa uzima unaozaa matunda aina 12, tena uko katikati ya mji utaleta uzima na ujana usiokoma kwa wale watakaoula..
5. Je, ni kweli mji huu wa ajabu utashuka hapa duniani?
“Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa
tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” Ufu. 21:2. “Heri wenye upole; maana
hao watairithi nchi.” Mt. 5:5. “Mwenye haki atalipwa duniani.” Mit. 11:31.
6. Jambo gani litatokea kwa dhambi na wenye dhambi?
“Watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza.”
Mal. 4:1. “Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.” Ufu. 20:9. “Viumbe vya asili vitaunguzwa,
na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.” 2 Pet. 3:10. “Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu.”
Mal. 4:3. “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani
yake.” 2 Pet. 3:13. Dhambi pamoja na wenye dhambi wataangamizwa
kwa moto. Moto huu utayeyusha dunia na kufanya kila kitu kiwe majivu..
7. Ni ahadi gani za kusisimua ambazo Mungu anatoa kwa watu
watakaoingia katika ufalme huu mpya?
A. Mungu mwenyewe ataishi pamoja nao (Ufu. 21:3).
B. Hakutakuwa na kifo tena, wala maumivu, machozi, huzuni, ugonjwa, hospitali, majanga, taabu, njaa na
kiu (Ufu. 21:4; Isa. 33:24; Ufu. 22:3; Ufu. 7:16).
C. Hawatachoka (Isa. 40:31).
D. Kila aliyeokolewa atakuwa na mwili mkamilifu kwa kila njia. Viziwi watasikia, vipofu wataona, mabubu
wataimba, na vilema watakimbia (Isa. 35:5,6; Flp. 3:21).
E. Hawatabughudhiwa. Watapata mema milele(Zab. 16:11).
F. Wivu, hofu, chuki, udanganyifu, husuda, uchafu,wasiwasi na uovu wote hautakuwepo katika ufalme
wa Mungu (Ufu. 21:8,27; 22:15).
8. Nchi mpya itakuwa na tofauti gani na dunia yetu ya leo?
A. Katika ufalme wa Mungu nchi yote itakuwa bustani nzuri yenye mito, maziwa mazuri na milima mizuri
(Ufu. 22:1)
B. Majangwa yatakuwa bustani (Isa. 35:1,2).
C. Wanyama wote watakuwa wapole. Hawatauana na mtoto mdogo atawaongoza (Isa. 11:6-9; Isa.65:25).
D. Hakutakuwa na laana tena (Ufu. 22;3).
E. Hakutakuwa na ukatili wa aina yo yote (Isa. 60:18), hii ni pamoja na uhalifu, dhoruba, mafuriko, matetemeko, tufani, majeraha, n.k.
F. Hakuna kinyonge kitakachoingia katika nchi mpya (Ufu. 21:27). Hakutakuwa na vichungi vya sigara,
walevi, vilabu, baa, pombe, ukahaba, picha za aibu, na uovu wala uchafu wa aina yo yote.
9. Je, kutakuwa na watoto katika ufalme wa Mungu? Na kama ni
hivyo watakuwa wanakua?
“Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.” Zek. 8:5.
10. Baada ya waliookoka kukutana na wapendwa wao kule mbinguni, je, wataweza kutambuana?
“Wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.” 1 Kor. 13:12.
11. Je, kule mbinguni, watu watakuwa ni watu halisi wenye mifupa na nyama?
“Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia,
Amani iwe kwenu. Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.” “Basi walipokuwa
hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa? Wakampa
kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao.” “Akawaongoza mpaka Bethania,… Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.”
Lk. 24:36-39,41-43,50,51. “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo
hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.” Mdo. 1:11.
“Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu.”
Flp. 3:20,21. Baada ya kufufuka, Yesu aliwathibitishia wanafunzi wake kuwa alikuwa na mwili wa nyama na mifupa kwa kuwaruhusu wamguse na kwa kula chakula. Wenye haki,
watapewa mwili kama wa Kristo, nao watakuwa watu halisi wenye mifupa na nyama milele zote..
12. Je, wenye haki watakuwa wakifanya nini katika ufalme wa
Mungu?
“Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake;
hawatapanda, akala mtu mwingine;… wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.”
Isa. 65:21,22. Watajenga nyumba katika nchi mpya, lakini kila mmoja atakuwa na jumba lililojengwa na Yesu katika mji; watalima na kula matunda. Watu halisi watakuwa
wakifanya mambo halisi katika nchi mpya. Na watayafurahia.
13. Waliokombolewa watajishughulisha na mambo gani mengine ya kusisimua?
A. Kuimba na kupiga muziki wa mbinguni (Isa. 35;10; 51:11; Zab. 87:7; Ufu. 14:2,3).
B. Kuabudu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kila Sabato (Isa. 66:22,23).
C. Kufurahia maua na miti isiyonyauka (Eze. 47:12; Isa. 35:1,2).
D. Kuongea na wapendwa wao, wazee wa imani, manabii, n.k. (Mt. 8:11; Ufu. 7:9-17).
E. Kumsikiliza Mungu akiimba (Zef. 3:17).
F. Kujifunza wanyama wa mbinguni
(Isa. 11:6-9; 65:25).
G. Kusafiri mbali na kufanya uchunguzi bila hata ya kuchoka (Isa. 40:31).
H. Kutimiza haja za moyo wao
(Isa. 65:24; Zab. 37:3,4).
I. Jambo la furaha kuliko yote – nafasi ya kuwa kama Yesu, kutembea pamoja naye na kumwona uso kwa uso (Ufu. 14:4; 22:4; 1 Yoh. 3:2).
14. Je, lugha dhaifu za wanadamu zinaweza kuelezea utukufu wa
makao ya mbinguni?
“Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,… Mambo ambayo Mungu aliwaandalia
wampendao.”1 Kor. 2:9.
15. Je, ufalme huu unaandaliwa kwa ajili yangu?
“Yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.” Ufu. 22:17. “Tupate na urithi usioharibika… uliotunzwa
mbinguni kwa ajili yenu.” 1 Pet. 1:4. “Naenda kuwaandalia mahali.” Yn 14:2. Umeandaliwa kwa ajili yako. Na Mungu anakukaribisha wewe mwenyewe binafsi. Ukiukosa
rafiki, hutakuwa na wa kumlaumu, isipokuwa wewe mwenyewe.
16. Nitahakikishaje kuwa ninapata nafasi katika ufalme huo mkuu
na wenye utukufu?
“Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake.”
Ufu. 3:20. “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.”
Ufu. 14:12. “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye
afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mt. 7:21. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu.” Yn 1:12. “Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” 1 Yoh. 1:7. Biblia iko wazi. Ni rahisi sana. Mpe Yesu maisha yako ili akutakase kutoka dhambini. Ukifanya hivyo, atakupa uwezo wa kufanya mapenzi yake na kuzishika
amri zake. Hii ina maana kwamba utaanza kuishi kama Kristo alivyoishi na utashinda dhambi zote. “Yeye
ashindaye atayarithi haya (Ufu. 21:7). Kwa kifupi, mtu anakuwa tayari kwa ajili ya kwenda mbinguni kama
mbingu imo moyoni mwake. Haya yote Yesu anayaandaa kwa ajili yako. Ukimpokea yeye yote yatakuwa yako. Je, umeamua sasa kumpokea Yesu
pamoja na zawadi yake ya uzima wa milele katika nchi mpya?
Ubarikiwe
Post a Comment