HAJI MANARA AVULIWA USEMAJI SIMBA SC, KLABU YARIDHIA
Klabu ya Simba SC, imemteua Ndugu Ezekiel Kamwaga kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu kwa kipindi cha miezi miwili.
Katika kipindi hicho, Kamwaga atashiriki katika maboresho ya muundo na utendaji wa Idara hiyo.
"Kamwaga ni mwandishi wa habari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 kwenye tasnia ya habari - akifanya kazi katika vyombo vya habari vya ndani na kimataifa"---- SIMBA SC
"Kamwaga anaijua vizuri Klabu ya Simba na historia yake kwani amewahi kuitumikia katika nafasi za Msemaji wa Klabu na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba"---- SIMBA SC
Wakati huo huo, Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, kwa kauli moja, imeridhia matakwa ya Ndugu Haji Manara ya kutoendelea kuhudumu katika nafasi ya Msemaji wa Klabu. .
Aidha, Bodi ya Simba SC inamshukuru kwa maneno aliyoyatumia kuwaaga wana-Simba katika kundi la viongozi wa Simba (Simba HQ) na kwa kazi aliyoifanyia Klabu katika kipindi
alichoshika nafasi hiyo, na inamtakia heri katika shughuli zake.
Mara baada ya kukamilika kwa maboresho ya Idara ya Habari na Mawasiliano na Idara nyingine, Klabu ya Simba SC, imepanga kutangaza fursa mbalimbali za ajira katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Post a Comment