SERIKALI YABAINISHA MAKUNDI KUPATA HUDUMA YA CHANJO
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeweka wazi makundi ya kipaumbele yatakayoanza kupata huduma ya Chanjo ili kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya COVID-19.
Makundi hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akiongea na Waandishi wa habari katika viwanja vya MUHAS Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa, kwa awamu ya kwanza Serikali imepokea jumla ya dozi 1,058,400 ambazo itaelekeza kuchanja makundi ya kipaumbele kwenye kila mkoa kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo wakiwemo watoa huduma za afya walio mstari wa mbele, watu wanaoshambuliwa zaidi na UVIKO 19 kama wenye magonjwa sugu na wenye umri wa miaka 50 na zaidi.
"kutokana na kuwa dozi ambazo serikali imepokea ni kwa awamu ya kwanza ni 1,058,400 hivyo, wataanza kuchanja makundi ya kipaumbele kwenye kila mkoa kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo kuwa ni pamoja na watoa huduma za afya walio mstari wa mbele, watu wanaoshambuliwa zaidi na UVIKO 19 wakiwemo wenye magonjwa sugu na wenye umri wa miaka 50 na zaidi" amesema.
Aliendelea kusema kuwa, makundi mengine yataendelea kupata huduma hii kwa kadri Serikali inavyoendelea kuingiza nchini dozi nyingine za chanjo ili kuendelea kuwakinga wananchi dhidi ya ugonjwa na vifo vitokanavyo na UVIKO-19.
Ameweka wazi kuwa, hadi kufikia tarehe 22 Julai, 2021 jumla watu 4,127,963 walishapoteza maisha duniani huku 191,773,590 wakiwa wamethibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO 19. Kwa upande wa Afrika kwa tarehe hiyo hesabu ya walioambukizwa lishafikia 4,583,414 na waliofariki 108,056.
Aidha, Dkt. Gwajima amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kitendo cha kuongoza uzinduzi wa mpango wa kuchanja ambacho kinaashiria uongozi wa ushujaa, uthubutu na uzalendo kwa taifa lake katika mapambano dhidi ya COVID-19.

Post a Comment