HAPPY BORN DAY PRIVALDINHO

ALWATAN ABDULAZEEZ;
Shukrani kwa Kahari, Jalali wetu Manani, 
Hakika mwenye kadiri, kutuweka salimini, 
Kaiweka hali shwari, katujalia amani, 

Katu hapandi farasi, yule mzoea punda,
Mpenda kwenda kwa kasi, mwendo pole humshinda,
Amezoweshwa fenesi, doriani lamshinda,
Sitokalifisha nafsi, tafanya utavyopenda, Simama ewe Priva, Tukupe maji upoe.

Halikua tabasamu la Bi Romana pekee bali hata kinywa cha mzee Abiudi hakikufumba hata kwa sekunde moja, kwasababu ya Furaha aliyoipata siku ya 13 ya mwezi Mei.

Kila mja alifahamu kuwa jembe limezaliwa, pasi na kuilaza damu, wazee hawa walihakikisha unapata Elimu ya maana. Chaguo sahihi lilikua pale Mwika high School kisha Maramba sec ambapo ulimaliza kidato cha nne.

Malangali Boys leo hii inajivunia wewe Priva, hakika unakitendea haki cheti chao cha Form 6. Si hao tu hata wanasheria wote UDOM ya pale Idodomya wanajipiga vifua na kujigamba, kwakua unawawakilisha vyema.

Keti pembeni Tuzungumze ewe farasi wa Vita, naomba nikukutanishe na Mvumbuzi mkubwa wa kule Amerika ya mbali. Huyu anaitwa Thomas A. Edson. Aliwahi kusema "Genius is one percent inspiration and ninety-nine percent perspiration"

Yani Genius hujengwa kwa 1% ya msukumo (ushawishi) pamoja na 99% za jasho. Hapa Nakuona wewe Priva. Kama lisingemwagila jasho lako la juhudi na ubunifu basi usingeimudu vita hii.

Kama lingekauka jasho lako ka uvumilivu, busara na upendo, leo hii tungepata wapi dodoso za kweli? Ama kweli Thomas Edson alimaanisha.

Mapambano yako tunayaona, juhudi zako tunazitambua na wengine tunajifunza, leo hii vijana wengi tunaaminika kwenye Nyadhfa mbali mbali, hii ni kutokana na juhudi zenu vijana mliyovalia Njuga Michezo.

Ewe Farasi mwongoza njia, tunajua upo vitani, kasi yako si ya kitoto, lakini Simama kwanza unywe maji na usherehekee siku yako ya kuzaliwa. Kisha utaendelea na vita hii katika Tasnia tunayoitumikia.

Happy Birthday broh @privaldinho
Adversity reveals genius, prosperity conceals it.

Privaldinho; Mungu akubariki bro kwa andiko lako

No comments