KUFIKIA MIEZI 18 IJAYO KERO YA MAJI ITAFUTIKA-MABULA
Wilaya ya Nyamagana inatazamiwa kutumia takribani Tsh. 152 BIL kwenye miradi mikubwa mitatu ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Maji.
Hayo yamebanishwa na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. @stanslaus_mabula wakati wa ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa katika Kata ya Lwanhima ambapo alipokea kero 89 katika mikutano ya hadhara 6 na kikao kimoja Cha Ndani.
Kero 51 zilijielekeza kwenye uhaba wa Maji na wananchi kuomba Visima vya Maji pamoja na mgao wa Maji angalau Mara Moja kwa wiki kero zingine ilikuwa ardhi, Fidia, Umeme, Dhuruma, ucheleweshaji wa Namba za NIDA, ukosefu wa Eneo la Masoko na Malalo, Huduma za Afya pamoja itirafu katika uwekaji wa Namba za anwani za makazi.
Mhe. Mabula ametumia adhra hizo kufafanua mipango madhubuti iliyowekwa na serikali ya CCM kuanzia awamu ya tano mpaka awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluh Hassan.
Mabula ameeleza, ujenzi wa Chanzo kipya Cha Maji Butimba ambacho kimepatiwa Bil 68, na bil 69 kwaajili ya upanuzi wa mradi wa Chanzo kipya Butimba pamoja na ujenzi wa matank makubwa ya Maji yenye uwezo wa kuhifadhi Lita mil 6 katika Maeneo mbalimbali ikiwemo Kata ya Lwanhima na Igoma.
Pia Mhe mbunge ameeleza serikali imetoa bil 17 ya ujenzi wa mtandao wa Maji utakaotoka katika Chanzo kipya Cha Maji Butimba, uwekeaji wa Kituo Cha Maji pamoja na Tank kubwa lililojengwa Kata hiyo eneo la Sawah lenye uwezo wa kubeba Lita mil 2, mengine yenye Lita mil 6 ambayo yataenda kuondoa Kabisa uhaba wa Maji.
Mhe. Mabula amesema, serikali inayodhamira ya dhati kuondoa changamoto ya uhaba wa Maji kwa Utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa ambayo inatazamiwa kukamilika mwaka 2023. Hivyo amewasihi wananchi kuwa na subira na kuahaidi kuzungumza na MWAUWASA ili liweze kuleta Pump ya Maji katika baadhi ya Visima ambavyo Pump zimeharibika.
Mhe. Mabula aliambatana na Diwani Kata ya Lwanhima, Wenyeviti wa Mitaa, Mjumbe Kamati ya siasa CCM Nyamagana Sanyenge, Katibu wa UVCCM wilaya ya Nyamagana Malanyingi Matukuta, Viongozi waandamizi wa CCM Kata wakiongozwa na Mwenyekiti Kata.

Post a Comment