KANDURU AMVAA GWAJIMA, AMTAKA AOMBE RADHI KWA SAMIA
"Ukiwa Mbunge wa CCM ni lazima Uheshimu taratibu za Kichama, kuna tabia ya baadhi ya Wabunge kwenda kwenye makongamano ya Kitaaluma na kuanza kukosoa Serikali Iliyopo Madarakani" Kanduru Mkt UVCCM, Mtwara.
"Kama unataka kukosoa acha huo Ubunge ukafanye harakati za kuikosoa serikali ya CCM nje ya Ubunge, lakini pia ifahamike kwamba Wabunge wanayo platform ya kuishauri CCM na Serikali yake kwa Utaratibu wa Kikanuni na Nidhamu kabisa" Kanduru, Mkt UVCCM Mtwara.
"Kitendo cha Gwajima kupinga na kudhihaki hadharani maelekezo ya M/kiti wa CCM Taifa Samia ni ukiuka mkubwa wa miongozo ya chama, hivyo nashauri Uongozi wa juu upitie kauli za Gwajima na kuchukua hatua"Kanduru, Mkt UVCCM Mtwara.
"Tunaiomba CCM kutafakari kwa kina uzito wa kauli za uchonganishi na kuwayumbisha Watanzania, na kejeli zilizotolewa na Gwajima na Ikiwezekana achukuliwe hatua za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kutotii mamlaka" Nasibu Kanduru Mk UVCM mtwara
"Gwajima ni Mbunge kupitia CCM na Wabunge wa CCM Wanaongozwa na Katiba ya CCM, Kanuni na taratibu Mbalimbali. Nyaraka hizo zote zimefafanua kuwa ni Mwiko kwa Mbunge wa CCM kupinga au Kutokufuata maelekezo ya Viongozi wa Chama" Kanduru, Mkt UVCCM Mtwara.
"Pia Gwajima awaombe radhi Wanachama wa CCM na Watanzania kwa ujumla kwa kauli zake za kudhihaki na kusema uongo kwa Watanzania kwa kuongea bila tafiti.Pia awaombe radhi waumini wake kwenye madhabahu aliyoyatumia kutoa kauli zake"Kanduru, Mkt UVCCM Mtwara.
"Nimuombe Mchungaji Gwajima kujitokeza hadharani kumuomba radhi M/kiti wa CCM Taifa na Rais Samia kwa kauli zake zisizo na staha na zenye kuligawa Taifa katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa COVID19" Nasibu, Mkt UVCCM, Mtwara.
"Mchungaji Gwajima amekwenda kinyume na Katiba ya CCM na Kanuni za Usalama na Maadili ambapo adhabu yake ni kufukuzwa Auanachama" Mkt UVCCM Mtwara.
"Gwajima lazima ajue yeye ni Mwanachama wa CCM na CCM imempa heshima kubwa ya kuwa Mbunge, hivyo kukejeri, kudhihaki na kupingana na msimamo wa Rais na m/kiti wa CCM Taifa Mhe. Samia kwenye ugonjwa wa COVID19 ni uhaini" Nasibu Kanduru, Mkt UVCCM Mtwara.
Post a Comment