TMDA YATAKA KUTENGA MAENEO MAALUM YA KUVUTIA SIGARA

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imetoa mwaka mmoja kuanzia jana Julai 26, 2021 kwa wenye maeneo panaporuhusiwa kuvuta sigara kutenganisha vyumba/maeneo maalum ya kuvutia na kutovutia sigara. 

Aidha, imetangaza ukaguzi kuanza kufanyika nchi nzima kuhakiki utekelezaji, na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao hawatotii.

No comments