KOCHA VAZ PINTO AJIUZULU KUITUMIKIA GOR MAHIA

Gor Mahia wamepata pigo kubwa wakati wa kusaka taji la FKF-Premier League baada ya kocha mkuu Vaz Pinto kujiuzulu jana usiku.

Katika mahojiano na Binago Blog, alitaja sababu za kibinafsi na "nyakati ngumu tofauti tofauti" kama sababu ambazo zimesababisha kuhama kwake ingawa ripoti ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha angeweza kujiunga na CD Nacional, timu inayoshiriki Primeira Liga nchini Ureno ambako ndiko alikozaliwa kocha huyo.

Pinto alijiunga na Gor Mahia mwanzoni mwa kipindi hiki na aliongoza klabu hiyo kutwaa taji la Kombe la FKF wiki iliyopita, akiifunga AFC Leopards kwenye mikwaju ya penati.

Mbali na taji la kombe anaondoka akiwa ameiongoza Gor Mahia kushika nafasi nne kwenye jedwali la timu 18 za FKF-PL akiwa amekusanya alama 39 kutoka katika michezo 23.

Mpaka sasa ameketi nyuma ya vinara wa Ligi;- Tusker (50), KCB (46) na AFC Leopards kwa 43.

No comments