KANISA LA TB JOSHUA LAUNGUA MOTO
Kumetokea mlipuko wa moto katika Kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote Jumatatu usiku, wakati wa mazishi ya mhubiri wa Nigeria Temitope Balogun Joshua maarufu kama Nabii TB Joshua.
Wakati mazishi yakiendelea huko Lagos, moto uliteketeza ghala katika majengo ya kanisa hilo mnamo saa 11 jioni.
Maafisa wa kanisa hilo walisema moto huo ulisababishwa na cheche ya umeme.
Post a Comment