SHEIKH MSELEM ASEMA MIHADHARA ILILENGA KATIBA MPYA

Sheikh Mselem Ali, mmoja kati ya Masheikh wa Uamsho ambao wametoka Gerezani amesema mihadhara yao ilikuwa na nia ya kuwaamsha watu kudai Katiba Mpya

Amesema kwa kipindi kile walifanya hivyo kwa kuwa kulikuwa na fursa ya maoni kuhusu Katiba Mpya. Walifanya hayo kwa Mujibu wa Sheria kwa kuwa Katiba inaruhusu kila mtu kutoa mawazo au maoni yake

Aidha, Sheikh Mselem amesema hana Chama cha Siasa na wala hana mamlaka ya kudai KatibaMpya lakini ikitokea Serikali inataka maoni kuhusu Katiba mpya na wakiona anaweza kuchangia mawazo basi atashiriki

No comments