SIMBA 𝗪𝗔𝗠𝗘𝗠𝗖𝗛𝗢𝗞𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗠𝗔


 Uchambuzi kutoka Clouds fm Sports Extra baada ya klabu ya Simba SC kumsimamisha kiungo wao, Clatous Chama. 


“Chama ni mchezaji aliyeipa mafanikio makubwa klabu ya Simba lakini naona sasa Chama yupo ukingoni, Simba na Chama wanasumbuana sana hasa katika kipindi cha usajili au ligi inapoenda mwishoni”


“Kwanza Chama siku zote utasikia anaidai Simba na ni mchezaji anayesajiliwa na timu nyingine kila usajili(wakati wa usajili lazima utasikia Chama anasajiliwa na timu fulani)”


“Amekuja Robertinho na akaonekana ana taratibu zake lakini baada ya kumfanyia sub watu walilaumu sana ,Robertinho akakaubali kuingia kwenye mfumo wa Chama”


“Robertinho ameondoka kaja huyu Benchikha ambaye amesema hapana lazima aingie kwenye mfumo ama zake ama zangu”


“Simba wanatafuta jinsi gani ya kumalizana na Chama , siku hizi Chama amepunguza uzalishaji klabuni lakini amekuwa na sintofahamu nyingi na Klabu”


“Mgogoro wa Chama na Simba haujaanza hivi sasa na kila mmoja kwa nafasi yake anaonekana yupo sahihi na Simba wanaonekana wanatafuta timing tu ya kuachana na Chama”


“Ndio maana kuna mechi Chama hakuanza lakini hakuna anayeuliza kwanini Chama hajaanza”SportsXtra | - @mastertindwa 


“Simba na Yanga wakimchoka mchezaji kuna namna wanafanya ,Yanga na Saido walimtoa chambo Ambundo wote walisimamishwa Ambundo akabaki Saido akaagwa”


“Hii ya Kapama na Chama ni kuambatanisha ,kwenye hili Kapama ni chambo tu mlengwa ni Chama”


@ Master Tindwa | Mchambuzi



“Ni mapema sana kufikiria huo mwisho wa Chama kwa huku kusimamishwa ,mimi ninachokiona Klabu na mchezaji kutokea changamoto ni kawaida ,imekuwa stori kubwa kwa sababu ni Chama”


“Hata ukienda ukatafiti kwenye NBC wachezaji waliosimamishwa sio Chama peke yake,hata kwenye hii taarifa ni Chama na Kapama. Kibaya zaidi hakuna ufafanuzi kuwa huo utovu wa nidhamu ni upi ?”


@ Yahya Njenge | Mchambuzi



No comments